Loading...

Sep 28, 2020

Polisi walazimika kutumia mabomu ya machozi kwenye msafara wa Lissu


 

Na Timothy Itembe Mara.

JESHI la polisiTarime Rorya wamelazimika kutumia mabomu ya mchaozi kunusuru msafara  wa mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana kuwa ni wafuasi wa chama gani.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya,ACP,Wilyamu Mkonda alisema kuwa leo asubuhi majira ya saa 5 polisi wa msafara wa mgombea urais wa Chadema walirushiwa mawe na watu wa siojulikana ambapo jeshi la polisi lililazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

“Wakati mgombea  huyo akizungumza na wananchi kundi la watu wasio julikana ni wafuasi wa chama gani walianza kuwarushia askari polisi waliokuwa kwenye msafara mawe hali iliyosababisha walazimike kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi ili kunusuru msafara wa mgombea”alisema Mkonda.  

Mkonda aliongeza kuwa mgombea huyo kwa leo haukuwa na ratiba ya kufanya mkutano  wilayani Tarime kwa mjibu wa  ratiba ya Tume ya uchaguzi iliyotolewa kwa wagombea wa vyama vya siasa.

Kamanda alifafanua kuwa ratiba ya mgombea urais wa Chadema  Tundu Lissu ilionyesha kuwa atafanya mkutano Serengeti akielekea Arusha ambapo msafara huo ungepitia Nyamwaga Nyamongo na kuelekea Serengeti ili kufika Arusha kuendelea na kampeni za uchaguzi.

Kamanda huyo alitumia nafasi hiyo kuvitaka vyama vya siasa na wagombea wao kufanya siasa kwa kuzingatia ratiba zilizotolewa na  Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Kamanda pia aliwataka wananchi na wafuasi wa vyama vya isasa kujiepusha na mihemko ya kisiasa inayoweza kuhatarisha uvunjifu wa amani.

Mkonda amemaliza kwa kusema kuwa katika tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu wanne  kwa upelelezi na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa sehemu husika.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger