Rais wa Belarus afanya ziara Urusi ili kupata mikopo zaidi na uungwaji mkono wa kisiasa


Rais wa Belarus ameitembelea Urusi katika juhudi za kupata mikopo zaidi na uungwaji mkono wa kisiasa wakati maandamano dhidi ya utawala wake wa miaka 26 yakiingia wiki ya sita.

Mazungumzo kati ya Alexander Lukashenko na Rais Vladmiri Putin wa Urusi yanajiri siku moja tu baada ya watu wanaokadiriwa kuwa 150,000 kufanya maandamano katika mji mkuu wa Belarus wa Minsk wakimtaka Lukashenko ajiuzulu.

Wizara ya mambo ya ndani imesema watu 774 wamekamatwa mjini Minsk pamoja na miji mingine kwa kushiriki mikutano isiyo na kibali mnamo siku ya Jumapili.Putin amesema Urusi itatoa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.5 kwa Belarus na kutimiza majukumu yake chini ya mkataba wa umoja kati ya nchi hizo jirani.

Putin pia amempongeza Lukashenko kwa ahadi yake ya kufanya mageuzi ya katiba.Hata hivyo upinzani umepuzilia mbali mazungumzo ya Lukashenko kuhusu mageuzi ya katiba wakisema ni njama tu ya kutuliza hasira za waandamanaji.

Post a Comment

0 Comments