Rais wa Peru anusurika kuondolewa madarakani na bunge

Rais wa Peru Martin Vizcarra amenusurika kuondolewa madarakani kupitia mchakato wa kura iliyopigwa bungeni jana Ijumaa. 

Wapinzani wame walishindwa kupata wingi wa kura zilizohitajika kumuondowa madarakani rais huyo. Bunge la Peru lilipiga kura wiki iliyopita ya kuanzisha mchakato wa kumuondowa madarakani kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57,kutokana na ukosefu wa maadili. 

Inadaiwa kwamba rais Vizcarra aliwachochea wasaidizi wake kutoa taarifa za uwongo kwa wachunguzi wa kupambana na rushwa. 

Rais Vizcara amedai spika wa bunge Manuel Marino aliyeanzisha mchakato huo ana njama ya kumuondowa madarakani kwa kujaribu kupata uungaji mkono wa jeshi.

Post a Comment

0 Comments