TAKUKURU Kiteto yaokoa mradi wa mil 27


 

Na John Walter-Kiteto.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imeokoa mradi wa mil 27, Kijiji cha Nalang’tomon Kata ya Partimbo, wilayani humo, uliohujumiwa miaka minne iliyopita na mdhabuni pamoja na baadhi ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji na kusababisha adha kwa wananchi.

Katika kipindi hicho wananchi waliendelea kutaabika namna ya kupata maji safi na salama na kujikuta wakitumia maji ya bwawa la Nalang’tomoni Kijijini hapo yanayotumiwa na mifugo kipindi chote.

Akikabidhi fedha kiasi cha Tsh mil 6.530,000 kati ya 9,000.000 zilizokuwa zimehujumiwa katika mradi huo toka kwa baadhi ya wajumbewa Serikali ya Kijiji pamoja na mdhabuni, Mkuu wa Takukuru Kiteto, Venance Sangau alisema mradi huo ulisimama toka mwaka 2016 muda mfupi baada ya Serikali kuukamilisha

“Tulipata taarifa kuwa wananchi wamehujumiwa mradi wao wa maji, tukafika na kuanza uchanguzi ambapo nimebaini wizi na hujuma kubwa iliyofanywa na baadhi ya wajumbe pamoja na mdhabuni wao hapo Kijijini na kuwataka wazirejeshe ambapo nakabidhi fedha hizo kwako mil 6,530,000 kati ya mil 9 ambazo zitakamilishwa ndani ya muda mfupi”alisema Sangau

Alisema miradi mingi ya maji Kiteto inahujumiwa kwa maksudi na baadhi wawakilishi wa wananchi, mfano mashine ya mradi huu ambao Serikali imegharamia mil 27 haionekani huku kukiwa hakuna maelezo ya kutosha huku mradi mwingine wa maji wajanja hao wakiwa wameanzisha pembenu na kufanya biashara ya maji

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Patrick Norbert Songea akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo alieleza kuwa naye amebaini hujuma wanazofanyiwa wananchi na baadhi ya watumishi wa Serikali pamoja na mamlaka ya maji na kutoa agizo miradi yote ikamilike tena kwa kiwango stahili

“Kwanza TAKUKURU Kiteto niwapongeze kwa kazi nzuri mnazofanya, pamoja na kwamba najua uchache wenu lakini kwa muda mfupi mmefanya kazi kubwa sana na zenye tija..mmewaondolea adha wananchi katika nyanja mbalimbali za huduma zao”

Naomba muendelee kufanya hayo kwani tutaungana pamoja, niagize pitieni miradi yote ya maji hapa Kiteto na chukueni hatua za haraka kisha mnipe taarifa kwani wananchi wengi wanalalamika kila kona, na mimi kama mwakilishi wa Rais hapa sitofumbia macho uozo huu alisema Kanali Songea

Wakala wa maji Kiteto Stephano Mbaruku baada ya kukabidhiwa fedha hizo ili aweze kwenda kurejesha huduma hiyo alimwahidi Mkuu huyo wa wilaya kuwa ndani ya mwezi mmoja atarejesha huduma ya maji kwa wananchi hao huku akikiri kuwepo wa ubadhirifu kwa baadhi ya miradi ya maji.

Kwa upande wake Hassani Swalehe (Mwananchi) Kijiji cha Nalangtomon alieleza adha wanayopata kuwa ni pamoja na kupatwa na magonjwa ya tumbo kwa kunywa maji ambayo sio safi na salama huku akiomba Serikali kuhakikisha kuwa wanawadhibiti viongozi ambao sio waadilifu.

Post a Comment

0 Comments