Ulaya kuyawekea vikwazo makampuni matatu kutokana na marrufuku ya silaha ya Libya

Jumatatu ijayo Umoja wa Ulaya unajiandaa kutangaza vikwazo dhidi ya makampuni matatu kutoka Uturuki, Jordan na Kazakhstan ambayo yanatuhumiwa kukiuka marufuku ya silaha nchini Libya. 

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa mwanadiplomasia ambae alizungumza na shirika la habari la Ufaransa la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina lake. 

Umoja wa Ulaya una mpango wa ulinzi bahari katika eneo la Pwani ya Libya, ambao una jukumu la kusimia utekelezaji wa marufuku ya silaha na kukusanya taarifa za wanaozikiuka. 

Uturuki ni moja ya wafadhili wakubwa wa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, yenye maskani yake mjini Tripoli, ambayo imekuwa katika mashambulizi kutoka kwa mbabe wa kivita anaendesha operesheni zake kutoka mashariki mwa Libya Khalifa Haftar.

Post a Comment

0 Comments