Wakazi wa Machimbo walia na ubovu wa Barabara

 


Wananchi wa Machimbo jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuwasaidia kufukiwa kwa mashimo makubwa ambayo yameachwa wazi mara baada ya kupitishwa kwa mabomba ya maji.


Wakiongea na EATV leo wananchi hao wamesema mashimo hayo licha ya kusababisha athari zikiwemo za watu kutumbukia lakini pia sasa yamegeuka kama ni mashimo ya kutupa taka huku mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Rahim Maridadi akieleza athari mbali mbali zitokanazo na mashimo hayo.


"Mashimo haya yana zaidi ya mwaka mmoja na nusu na yamekuwa yakisababisha wananchi kutumbukia na kuvunjika viungo vyao jambo ambalo linapaswa kushughulikiwa haraka ikiwemo kuzibwa",amesema mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Machimbo Rahim Maridad

Post a Comment

0 Comments