https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wizara ya Fedha kuanza kutoa Elimu ya uelewa matumizi ya GePG kwa wananchi | Muungwana BLOG

Wizara ya Fedha kuanza kutoa Elimu ya uelewa matumizi ya GePG kwa wananchi


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inatarajia kuanza kutoa elimu ya matumizi wa malipo ya serikali kwa njia ya Mtandao GePG kwa wananchi ili kuongeza uelewa kwa jamii juu ya matumizi ya mfumo huo mpya ambao umeleta mafanikio katika kukusanya mapato ya Serikali.

July 2017  Serikali ilizindua rasmi mfumo wa malipo ya makusanyo ya serikali kwa njia ya mtandao Government Electronic Payment Gateway GePG ambapo makusanyo yote ya Halmashauri na Taasisi za  kiserikali hutumia kukusanya mapato yake.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James wakati wa mkutano wa tathmini ya matumizi ya mfumo huo tangu kuanza kutumika hapa nchini ambapo amesema mfumo huo umekuwa na mafanikio katika kukusanya mapato.

Amesema mfumo huo bado umekuwa changamoto kwa wananchi hasa uelewa Kati ya  GePG na Control number wengi wamekuwa wanashindwa kutofautisha.

" Wananchi wengi wanatumia mfumo huu na unawasaidia lakini wengi hawaelewi maana ya GePG na Control number wengi wanasema nimetuma kwa kutumia Control number tutapita maeneo mbalimbali kutoa elimu hiyo wajue" amesema Dotto James.

Amesema mfumo huo umerahisisha kazi katika maeneo mbali mbali ambapo umesaidia kuondoa changamoto nyingi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na mfumo huo Sasa unatumiwa na taasisi zaidi ya mia sita (600).

Amebainisha kuwa tangu kuanza kwa mfumo huo ukusanyaji wa mapato ya Serikali umeimarika Sana hadi kufikia asilimia 250 na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

" Kabla ya mfumo huo tulikuwa tunakusanya bilioni 688 lakini kwa Sasa baada ya kuanza kwa mfumo huu tumefikia tilioni 2.6" amesema.

Aidha ameonya kwa taasisi na halmashauri zote hapa nchini kutoanzisha mfumo wowote bila idhini ya Waziri wa Fedha na Mipango ili kudhibiti uanzishwaji wa mifumo kiholela.

Amesema Wizara imeweza kutengeneza mifumo minne katika Kudhibiti mapato ya Serikali na imeanzisha  GePG, mfumo wa usimamizi wa matumizi ya Serikali MUSE, Mfumo wa usimamizi wa miradi ya maendeleo (kanzi data ya miradi ya maendeleo) na mfumo wa usimamizi wa misamaha ya kodi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Kwa upande wake mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu Cha Dar es saalam, UDSM, Profesa Dkt Joel Mtebe, amesema wamefanya utafiti kuhusu mfumo huo na kubainisha kuwa umekuwa msaada na kuwezesha ukusanyaji mzuri wa mapato ya Serikali.

"Tumepita maeneo mengi tumeona imekuwa msaada mkubwa na umedhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kuwawezesha watumishi katika maeneo yao kufanya kazi kwa wakati" amesema Dkt Mtebe.

 

Post a Comment

0 Comments