Aunty Ezekiel kumtaja mwanaume aliyempa ujauzito

 


Mwigizaji wa kike nchini, Aunty Ezekiel amesema wakati wowote atamtaja baba aliyempa ujauzito alionao kwani amekaribia kujifungua.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi, nyota huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aliyezaa na mmoja wa ma-dancer wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, alisema muda wowote ataonekana mwanaume aliyempa mimba.

Hata hivyo kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwamba mrembo huyo anatoka kimapenzi na baba mtoto wa msanii Ruby, Salmin Ismail ‘Kusah’ licha ya wenyewe kwa nyakati tofauti kukanusha habari hizo.

Lakini watu wao wa karibu wamekuwa wakisema wawili hao ni wapenzi na wanatarajia kupata mtoto.

Kusah mara zote amekuwa akisema Aunt ni rafiki wake na wanapeana sapoti katika kazi zao. Alisema ana mpenzi wake anayempenda na muda ukifika atamtambulisha hadharani ila hakutaja ni nani.  

Licha ya hao wote kuficha, rafiki wa karibu wa Aunt, #IreneUwoya aliamua kuweka mambo hadharani baada ya kuulizwa anamuitaje #Kusah na kusema ni shemeji yake kwa Aunt na hivyo, ndivyo anavyojua.


Post a Comment

0 Comments