Oct 13, 2020

Kim Jong Un amwaga machozi akiomba msamaha wananchi

  Muungwana Blog 3       Oct 13, 2020


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amewaomba radhi wananchi kwa matatizo yaliyokuwepo huku akitokwa na machozi.

Katika hafla ya maadhimisho ya miaka 75 ya chama tawala cha wafanyikazi nchini Korea Kaskazini, Kim Jong Un alishindwa kuzuia machozi alipokuwa akiomba msamaha wananchi kwa kutoweza kusimama taifa wakati wa misukosuko ya janga la virusi vya corona.

Kulingana na taarifa za Korea Times, iliarifiwa kuwa Kim Jong alimtaja babu yake na baba yake, na kusema, ‘‘Natoa shukrani kwa wananchi kwa kuniamini na kunipa jukumu la kusimamia dhamira za wakubwa wetu Kim Il-sung na Kim Jong-il. Lakini juhudi zangu hazikutosha kuokoa wananchi kutoka kwenye matatizo. Wananchi waliniamini kwa kiasi kikubwa mno. Lakini nilishindwa kukidhi matakwa yao. Naomba mniwie radhi kwa hili.’’

Miongoni mwa matatizo ya wananchi wa Korea Kaskazini aliyozungumzia Kim Jong kwenye hotuba yake ni, masaibu makubwa, shida zisizoisha na misukosuko ambayo haijawahi kutokea.

logoblog

Thanks for reading Kim Jong Un amwaga machozi akiomba msamaha wananchi

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment