https://monetag.com/?ref_id=TTIb Lissu aahidi kuboresha sekta ya uchumi | Muungwana BLOG

Lissu aahidi kuboresha sekta ya uchumi

 


Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema Serikali yake itaboresha sekta zote za kiuchumi, kikiwamo kilimo, uvuvi na maslahi ya watumishi wa umma, iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.


Mgombea Urais huyo wa Chadema, Tundu Antipas Lissu, ameyasema hayo alipohutubia mkutano wake wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Mnada wa Ng'ombe, Mjini Bariadi, mkoani Simiyu.


“Tutajenga nchi ya watu huru, tutajenga nchi ya watu wenye haki tutajenga nchi yenye maendeleo ya watu,wavuvi wote ni kilio cha kuumizwa cha kuchomewa mitumbwi yao, wakulima wa pamba ni kilio , nimekuja hapa ndugu zangu bariadi kuwaomba mnipigie kura niwe raisi wenu”  alisema Tundu Lissu


Katika hatua nyingine, Tundu Lissu, amebeza utaratibu uliotumika kuandaa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo machinga, huku akitaka pia Uchaguzi kuwa wa huru na haki.

Post a Comment

0 Comments