Maeneo 10 ambayo ni marufuku kubusu au kukumbatiana hadharani

 

Wakati kwenye maeneo mengine kubusu au kukumbatiana kati ya mwanamke na mwanaume ni jambo la kawaida, kwenye maeneo mengine ni kosa kubwa.

Baadhi ya nchi za kimagharibi zimewapa raia wake uhuru kiasi cha kuweza hata kufanya matendo ya faragha hadharani. Lakini baadi ya nchi, hasa zile zenye misingi imara ya kidini, zimepiga marufuku kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani.

Kwa kuwa lengo letu ni kukupa maarifa, basi fahamu maeneo 10 ambayo ni marufuku kubusu au kukumbatiana baina ya mwanamke na mwanaume hadharani.

1. Qatar

Qatar ni nchi yenye utamaduni wa Kiislamu ambayo hairuhusu mtu kubusu au kukumbatiana hadharani. Hata hivyo matendo haya baina ya wanafamilia au marafiki wa jinsia moja (wasio mashoga) siyo jambo baya.

2. India

Kwa mujibu wa sheria za India, mtu atakayekutwa akifanya au kuonyesha maswala ya kimapenzi hadharani anaweza kukabiliwa na kifungo kisichopungua miezi mitatu pamoja na faini.

3. China

Kutokana na utamaduni wa China, kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani ni kinyume cha maadili.

4. Dubai

Dubai ni mji ulioko katika falme za Kiarabu ambao sheria zake zinazuia watu kuonyesha hisia au kufanya matendo ya kimapenzi hadharani.

5. Thailand

Thailand ni nchi nzuri ya kuvutia hasa kwa utalii, lakini swala la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani halikubaliki katika maeneo mengi.

6. Indonesia

Unaweza ukatembelea fukwe na maeneo yenye vivutio mbalimbali nchini Indonesia; lakini uwe makini na swala la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani kwani halikubaliki.

7. Vietnam

Pamoja na mabadiliko mbalimbali kwenye utamaduni wa Vietnam, bado maeneo mengi hasa ya vijijini hayakubaliani na swala la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani. Unaweza usilishuhudie hili hadi pale utakapotoka nje ya miji mikubwa kama vile Hanoi na Saigon.

8. Chuo Kikuu cha Zimbabwe

Kwenye chuo kikuu cha zimbabwe, mwanafunzi anaweza kufukuzwa chuoni kwa kosa la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani. Hairuhusiwi kubusu, kukumbatia au hata kukaa kimapenzi katika viunga vya chuo.

9. Misri

Kwa kupitia tovuti ya Egyptian Streets, mwanadada Farah anaeleza jinsi alivyokutana na wakati mgumu kumkumbatia au kumbusu mpenzi wake wa Misri waliekutana huko Ulaya.

Ni wazi kuwa kanuni za Misri haziruhusu kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani.

10. Iran

Iran ni nchi nyingine ambayo ina misingi mikubwa katika imani ya Kiislamu, imepiga marufuku kufanya matendo kama vile kubusu au kukumbatia hadharani.

Neno la Mwisho

Ikiwa basi unataka kutembelea nchi hizi pamoja na mpenzi wako au unatarajia kupata mpenzi toka kwenye nchi hizi; ni vyema ukajihadhari kubusu au kukumbatiana hadharani kwani unaweza kuingia kwenye matatizo makubwa.

Post a Comment

0 Comments