Loading...

Oct 13, 2020

Nina uvumilivu ila ipo siku nitaongea- Mume wa Queen Darleen


 Baba Balqis! unaweza muita hivyo kwa sasa, ambaye ni mume halali wa ndoa na msanii Hawa Abdul, Queen Darleen ameahidi kufunguka (ya nyuma ya pazia) watu wanavyo mchukulia mkewe na namna wanavyoongea juu ya ndoa yake pasipo kujua mambo ya ndani.

Wawili hao ambao mwishoni mwa wikiendi iliyoisha wamebarakiwa kupata mtoto wao wakwanza wakike, waliyempa jina #Balqis, Isihaka kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza, Thamani ya mkewe anaijua yeye hivyo anawaacha waongee na siku wakijua ukweli wa mambo yote watabaki vinywawazi.

"My Wife @queendarleen_ Mama @balqis.isihaka Hongera na Pole ila najua watu wengi hawakujui wanakuona tu kwenye mitandao na kila mtu anaongea lake.

Thaman yako kwangu naijua mimi ila waache waongee na nikiamua kuongea mimi wakijua ukweli kila mtu ataacha mdomo wazi kwa vitu ntakavyoongea. Ila nashukuru mungu nimeumbwa na uvumilivu wa kutoongea mambo ya ndan ya Familia ila itafika muda ntaongea! #DontGiveUp #NoRespectNoLove

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger