RC Byakanwa “Atakaeleta vurugu siku ya uchaguzi kukiona chamoto”


 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.


Kuelekea uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020 siku ya jumatano  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametoa rai kwa yeyote atakayeleta vurugu hatua za kisheria zitamshughulikia.

Amesema hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema  amepata taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya kikundi cha watu ambacho kimepanga kuleta vurugu siku ya uchaguzi.

“Hali ya usalama ya Mkoa upo shwari imeendelea kuimarika ,nitoe wito kwa wananchi mliojiandikisha kujitokeza hiyo tarehe 28 kwa maana keshokutwa,tunazo taarifa za badhi ya watu na vikundi ambavyo wamejipanga kufanya vurugu ,mimi niwaambie tumejipanga na hawatafanya hizo vurugu”

Lakini pia Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi waliojiandakisha kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka.

Aidha Byakanwa amesema kuwa kwa Mkoa wa Mtwara  jumla ya wapiga kura laki tisa thelathini elfu mia nane arobini na moja  wamejiandikisha kupiga kura lakini pia kuna jumla ya vituo 2,753  na tayari vifaa vyote vimekamilika vya kupigikia kura.

Amechukua fursa hiyo kwa kutoa rai kwa wananchi mara baada ya kupiga kura ni vyema kurudi nyumbani ili kusubiri matokeo.

Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili na kufungwa saa kumi kamili ya jioni.

Post a Comment

0 Comments