Watu wa instagram wampa stress Gigy Money


Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amefunguka kuwa kuna watu wa aina tatu wanaotumia mtandao wa Instagram na wote wanaotumia mtandao huo ni 'stress' tu.

Gigy Money kupitia ukurasa wake wa Instagram ameainisha watu hao. Amendika sifa ya kwanza ya watu wanaotumia Instagram ni wale watakao like picha au video yako kwa ‘account zao’ ila comments zao zitakufanya u-log out, kisha anakulia maarage na ubwabwa na anasema akimaliza hapa anaenda kwenye page ya Gigy namchefua.

Kwenye sifa ya pili Gigy Money ameeleza kuwa, “Kuna wale ‘too class’ ushuzi wanajifanya hawataki watu waone like zao kama ni chakula au likes zao zitaongeza ‘filter’ kwa hiyo wana kurasa feki ‘fake page’ zao wanajifanya za biashara”

Aidha akimalizia sifa ya tatu ameandika kuwa, “Halafu kuna hawa ambao kama hawapo wao nikutumiana ‘DM’ naku-save matukio, sasa huko DM mnatunyambua kama nyinyi mnaweza kuvumilia, pia hawa wakutumiana DM ni wambea sana”.

Baada ya kuainisha sifa hizo za aina ya watu wa Instagram Gigy Money akamaliza kusema watu wa Instagram ni ‘stress’ tu.

Post a Comment

0 Comments