https://monetag.com/?ref_id=TTIb Saudia yakanusha mkutano kati ya Netanyahu na mrithi wa mfalme | Muungwana BLOG

Saudia yakanusha mkutano kati ya Netanyahu na mrithi wa mfalme

 


Saudi Arabia imekanusha ripoti kwamba kulikuwa na mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyedaiwa kufanya safari ya siri hadi taifa hilo la Kifalme wakati mrithi wa mfalme Mohamed bin Salman alipokutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan amesema ameona ripoti kwenye vyombo vya habari kuhusu mkutano huo, lakini hakuna mkutano kama huo uliofanyika. 

Na kwamba maafisa pekee waliokuwepo ni wa Marekani na Saudi Lakini afisa mmoja wa Israel amesema Netanyahu alisafiri hadi Saudi Arabia na alikutana na mrithi wa mfalme. 

Hiyo huenda ikawa uthibitisho wa kwanza wa hadharani kuhusu ziara hiyo, mnamo wakati mataifa hayo yakijaribu kuboresha uhusiano wao dhidi ya Iran.

Awali, kituo cha redio kinachomilikiwa na serikali nchini Israel pamoja na vyombo vingine viliripoti kuwa mkutano kati ya Netanyahu na Mohammed bin Salman pamoja na Pompeo ulifanyika Jumapili.

Saudi Arabia bado imekataa kurejesha mahusiano yao na Israel katika hali ya kawaida.


Post a Comment

0 Comments