Biden ateua timu ya wataalamu wa kiuchumi


Rais mteule Joe Biden ambaye alishinda uchaguzi wa urais nchini Marekani, ametangaza kumleta Gavana wa zamani wa Shirika la Fedha la Marekani (Fed) Janet Yellen kwenye Idara ya Hazina.

Biden alianzisha shughuli ya uteuzi na uzinduzi wa timu yake itakayosimamia na kuishauri idara ya uchumi huko Wilmington.

Biden, ambaye aliahidi "kufufua uchumi" na "kuhakikisha misaada" kwa wananchi wa Marekani, alihimiza bunge la serikali kupitisha sheria ya kifurushi cha misaada ya kiuchumi.

Akibainisha kuanzisha timu ya uchumi ya "daraja la kwanza" na “yenye uzoefu" ambayo itasaidia Marekani kujitoa kwenye mgogoro wa kiuchumi unaoendelea na kusaidia kujenga uchumi, Biden alisema atamleta Gavana wa zamani wa Fed Janet Yellen kusimamia Idara ya Hazina.

Janet Yellen atakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hiyo endapo uteuzi huo utaidhinishwa na Baraza la Seneti la Marekani.

Biden pia atamteua Neera Tanden mwenye asili ya India kuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Bajeti na Usimamizi wa Ikulu, na Cecilia Rouse kama Mwenyekiti wa Baraza la Washauri wa Uchumi.

Post a Comment

0 Comments