China ina matumaini ya kuboreka mahusiano yake na Marekani

 


China leo imempongeza rais wa Marekani Joe Biden aliyeapishwa jana kuchukua hatamu za uongozi na kutoa wito kurekebishwa mahusiano kati ya Beijing na Washington baada ya miaka minne ya uhasama chini ya Donald Trump. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China Hua Chunying amewaambia waandishi habari mjini Beijing, kuwa wito wa kuwepo umoja uliotolewa na Biden jana, ndiyo jambo linalohitajika kwenye mahusiano ya pande hizo mbili. 

Msimamo mkali wa utawala wa Trump dhidi ya China katika masuala ya biashara, haki za raia, janga la virusi vya corona na nguvu za kijeshi ulichochea kudodora kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya madola hayo mawili yenye nguvu. 

Ingawa Biden anatarajiwa kuendeleza msimamo mkali wa nchi yake kwa China, lakini atatumia lugha laini na kujaribu kufanya kazi pamoja na taifa hilo la mashariki ya mbali kwenye masuala ya kimataifa.


Post a Comment

0 Comments