Mambo matano usiyoyafahamu kumhusu Joe Biden

Mwanachama wa Democrat mwenye umri wa miaka 78 alichukua madaraka siku ya Jumatano katika hafla isiyo ya kawaida kwa sababu ya hatua kubwa za usalama ambazo zilipitishwa kuzuia mashambulio na uwezekano wa kutokea vurugu.

Biden, ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Marekania wakati wa utawala wa Barack Obama, anarudi Ikulu na jukumu la haraka la kushughulikia mgogoro wa kiafya na kiuchumi vinavyosababishwa na janga la virusi vya corona.

1. Siasa

Joe Biden aliingia katika siasa wakati wapiga kura wengi wa leo walikuwa hawajazaliwa.

Kazi yake huko Washington DC ilianza katika Seneti mnamo 1973, ambapo alishinda kiti kwa jimbo la Delaware akiwa na miaka 30 tu.

Kuwasili kwake katika siasa kuliambatana na moja ya wakati mbaya zaidi wa maisha yake, ambayo tutazungumza baadaye.

Akiwa seneta, Biden alijiimarisha kuwa mwanasiasa wa karibu, mpatanishi na mwenye uwezo wa kufikia makubaliano na wapinzani wake.

Alifanya pia maamuzi ambayo hayakupongezwa sana, kama sheria ya haki ya jinai ya 1994 aliandika na kupitisha wakati wa utawala wa kwanza wa Bill Clinton.

Marekebisho hayo yalilenga kupunguza machafuko yaliyozidi miongo kadhaa, lakini ilisababisha kufungwa kwa watu wengi, na athari kubwa kwa watu weusi na Walatino.

Kwa kazi yake ya muda mrefu ya seneta, lazima tuongeze miaka yake nane akiwa Makamu wa Rais wa Obama (2009-2017), ambaye alijenga uhusiano mzuri zaidi.

Urafiki kati ya Obama na Biden ulinaswa katika picha nyingi za utawala wake na wakati uliofuata.

Hii ilikuwa mara ya tatu kwamba alijaribu kuwa Rais wa nchi hiyo.

2. Janga lililotikisa safari yake ya kisiasa

Kwa bahati mbaya, furaha ya kushinda uchaguzi wa Seneti haikudumu kwa muda mrefu.

Wiki chache baada ya ushindi wake, familia yake ilipata ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa Washington, DC, akihojiana na wafanyakazi wa ofisi yake mpya.

Mkewe Neilia na watoto watatu wa wenzi hao walikuwa wakirudi kutoka kununua mti wa Krismasi wakati lori lilipogongana na gari lao.

Mwanamke huyo, 30, na binti mdogo, Naomi, mwenye miezi 13, walifariki.

Mke wa kwanza wa Biden, Neilia, alifariki pamoja na binti mdogo wa wenzi hao katika ajali ya gari.

Watoto - Beau, 3, na Hunter, 2, walijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitalini, lakini walinusurika.

Kipindi cha tofauti cha uchungu kilianza katika maisha ya Biden.

3. Maumivu

Biden, ambaye alikula kiapo katika ofisi ya Seneti katika chumba cha hospitali ambapo mtoto wake Beau alikuwa amelazwa, hakujua ikiwa ataendelea na kazi yake kama seneta.

''Nilivunjika moyo''.

Alilelewa katika familia ya Kikatoliki ya wafanyakazi, baba yake alikuwa akimpa moyo wa kusonga mbele.

Ndivyo alifanya. Aliamua kujitupa kazini, lakini bila kuacha watoto wake.

Joe na Jill Biden walioana miaka 40 iliyopita.

Katika miaka yake ya kwanza akiwa seneta: kila siku alifanya safari ya kwenda na kurudi kwa gari moshi kati ya nyumba yake huko Wilmington, Delaware, na Washington DC, zaidi ya kilomita 300 kwa siku kuwa karibu na yake .

Hivi ndivyo Biden alivyoanzisha uhusiano wa karibu na watoto wake ambao uliimarika tu walipokuwa watu wazima.

Mnamo 1977, Biden alimuoa Jill, profesa wa chuo kikuu ambaye ana binti, Ashley, na ambaye aliweza kujenga familia yake na yeye.

Wengi walimwona Beau kama mrithi wa baba yake katika siasa.

Baada ya kutumikia Iraq na Jeshi la nchini humo mnamo 2008, Beau alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Delaware.

Beau Biden alikuwa na umri wa miaka 46 alipopoteza maisha mwezi juni mwaka 2015.

Lakini mnamo 2013 aligunduliwa na aina nadra ya uvimbe wa ubongo na akafariki miaka miwili baadaye.

Kupoteza watu kama hao wa karibu kulimbadili Biden.

Wale wanaomjua vizuri wanasema kwamba ana "nguvu kubwa ya uelewa", tabia ambayo iliangaziwa wakati wa kampeni na tangu ushindi wake wa uchaguzi kumwasilisha kama mtu anayefaa kuponya majeraha na kuiunganisha tena nchi.

4. Uwajibikaji duniani

Biden ametetea hitaji la kujenga upya uhusiano wa Marekani na nchi washirika ambazo, kwa maoni yake, zimeathiriwa wakati wa urais wa Trump.

Anaahidi kurudi kwenye mkataba wa Paris kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kwa Shirika la Afya Ulimwenguni, kwa mfano.

Hakosi uzoefu: aliongoza Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti na anajivunia kwamba "amekutana na viongozi wote muhimu wa ulimwengu katika miaka 45 iliyopita."

Maamuzi yake katika nyanja ya kimataifa hayaja kuwa bila kukosolewa.

Mnamo 1991 alipiga kura dhidi ya Vita vya Ghuba; Hatahivyo mwaka 2003 alikuwa akiunga mkono uvamizi Iraq na baadaye akawa mkosoaji wa ushiriki wa Marekani katika nchi hiyo.

Alimshauri Obama asifanye operesheni ya vikosi maalum ambayo ilimalizika kwa kifo cha Osama Bin Laden.

Republican wanapenda kusema kwamba Robert Gates, Waziri wa zamani wa ulinzi wa Obama, alisema "hakuna njia mtu yeyote kutompenda Biden," lakini kwamba amekuwa "akikosea karibu kila sera kuu ya kigeni ya masuala ya usalama wa kitaifa. Katika miongo minne iliyopita. "

Gates hivi karibuni alibainisha kuwa maneno yake yalitafsiriwa nje ya muktadha.

5. Upinzani

Wapinzani wa Biden wanasema yeye ni wa zamani aliyepitwa na wakati, mzee sana.

Mtindo wake wa kuwa mtu mwenye msimamo umemsababishia shida, kama vile wakati aliposema katikati ya kampeni kwamba ikiwa Mwafrika-Mmarekani hakushawishika kumpigia kura ilimaanisha hakuwa mweusi, kauli ambazo baadaye aliomba msamaha.

Joe Biden amekuwa rais na aliyepata kura nyingi katika historia ya Marekani

Ingawa wapinzani wake wa Republican walijaribu kumuonesha kama mtu aliye na shida ya kiakili Biden alifanikiwa kupuuza na kuwa rais aliyepigiwa kura zaidi katika historia ya Marekani.

Cha kufurahisha, wakati wa kutathmini miaka michache iliyopita ikiwa au alihimizwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha urais 2016, Biden alisema: "Ninaweza kufa mtu mwenye furaha bila kuwa rais."


 

Post a Comment

0 Comments