Nyoni, Bocco nje, taifa stars ikiivaa Namibia leo

 


Timu ya taifa ya Tanzania ‘taifa stars’ itaendelea kuwakosa nyota wake John Bocco,Ibrahim Amen na Erasto nyoni walioripotiwa kuwa majeruhi, wakati ikitarajiwa kutupa karata yake ya pili kwenye michuano ya CHAN mchezo wa kundi D leo usiku dhidi ya timu ya taifa ya Namibia, utakaochezwa Saa.


Taifa stars ilipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 na timu ya taifa ya Zambia, na sasa kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mrundi Etienne Ndayiragije kinahitaji matokeo ya ushindli kwenye mchezo wa usiku wa leo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye fainali hizo za CHAN.


Namibia wao ndio wanaburuza mkia kwenye kundi hilo baada ya kufungwa mabao 3-0 na timu ya taifa ya Guinea kwenye mchezo wa kwanza, hivyo Taifa stars wapo juu ya Namibia kwenye msimao wa kundi wakiwa nafasi ya 3 kutokana na tofauti ya mabao ya kufungwa, Guinea ndio vinara wa Kundi D wakiwa na alama 3 sawa na Zambia, Guinea wakikaa kileleni kwa faida ya mabao ya kufunga.


Mara ya mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa Machi 5, 2014. mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Post a Comment

0 Comments