Malalamiko ya kuchelewesha chanjo Ulaya


Jumuiya ya Ulaya (EU) imetoa malalamiko juu ya kucheleweshwa kwa utoaji chanjo ya Oxford-AstraZeneca dhidi ya corona (Covid-19), ambayo bado haijaidhinisha kutumiwa.


Mhusika mkuu wa Tume ya EU ya mausala ya afya, Stella Kyriakides, alitoa maelezo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii baada ya kufanya mkutano wa kamati na wawakilishi wa nchi za EU juu ya mkakati wa chanjo.


Akifahamisha kuwa wawakilishi wa AstraZeneca walitangaza kwamba kutakuwa na ucheleweshaji wa utoaji chanjo kwa EU katika robo ya kwanza ya mwaka, Kyirakides alisema,


"Tume ya EU na nchi wanachama zilielezea kutoridhishwa na hali hiyo."


Kyirakides pia alisema kuwa EU inasisitiza juu ya kubainisha ratiba kamili ya uwasilishaji wa chanjo kulingana na idhini, kwa kuwa nchi wanachama zimepanga michakato yao ya chanjo kwa kuzingatia mpango huo.


Maombi yalitolewa kwa Wakala wa Dawa barani Ulaya (EMA) juu ya idhini ya chanjo ya AstraZeneca iliyozalishwa na Chuo Kikuu cha Oxford pamoja na kampuni ya dawa ya Uswidi na Briteni. Idhini ya EU ya chanjo hiyo ilitarajiwa kutolewa mwishoni mwa Januari.


Chanjo zilizotengenezwa na BioNTech, Pfizer na Moderna, ambazo zimeidhinishwa EU hadi sasa, zimekuwa zikitolewa kwa umma tangu Desemba 2020.


Tume ya EU imefikia msimamo wa kupokea takriban dozi bilioni 2.3 za chanjo kufuatia mikataba 6 iliyofanywa kwa niaba ya nchi wanachama na kampuni za uzalishaji wa chanjo hadi sasa. EU imesaini mikataba ya kununua dozi milioni 600 na BioNTech-Pfizer, milioni 400 na AstraZeneca, milioni 300 na Sanofi-GSK, milioni 400 na Johnson&Johnson, milioni 405 na CureVac na milioni 160 na Moderna. Hata hivyo bado kuna malalamiko kwamba mchakato wa chanjo unaendeshwa pole pole.

Post a Comment

0 Comments