Uturuki yatuma salamu za rambirambi Madrid


 Uturuki imetuma salamu za rambirambi baada ya mlipuko kutokea na kusababisha vifo Madrid nchini Uhispania.

Taarifa iliyoandikwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya nje, ilieleza kuwa Uturuki imepokea kwa habari kwamba watu wamepoteza maisha na kujeruhiwa katika mlipuko mbaya huko Madrid.

"Tunatoa pole kwa watu wa Uhispania na Serikali nzima kwa ujumla na kuwaombea rehma za Mwenyezi Mungu wale waliopoteza maisha.Tunawaombea shifaa wale wote waliojeruhiwa." iliongeza taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa za awali, watu 2 wameripotiwa kufariki kwenye mlipuko uliotokea katika jengo moja lililoko katikati mwa mji mkuu wa Madrid nchini Uhispania.

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa 15:00 (17:00 kwa saa za Uturuki) kwenye jengo la nyumba katika kitongoji cha Puerto de Toledo mjini Madrid.

Kulingana na picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, jengo hilo lilikumbwa na uharibifu mkubwa kutokana na mlipuko huo.

Vyombo vya habari vya ndani vimedai kwamba mlipuko huo unaweza kuwa umetokana na uvujaji wa gesi.

Post a Comment

0 Comments