WHO yatangaza kumalizika kwa janga la Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo


Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza kuwa wimbi la 12 la janga la Ebola lililoanza miezi 3 iliyopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limekwisha.

Taarifa iliyoandikwa kutoka WHO ilipongeza mafanikio ya maafisa wa afya wa DRC na wafanyikazi kwa juhudi zao katika janga hilo na makabiliano yao ya haraka.

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa wimbi la 12 la janga limeisha kuanzia leo, ingawa bado kuna haja ya kuwa makini na kudumisha mfumo thabiti wa uchunguzi wa kiafya.

Matshidiso Moet, Mkurugenzi wa WHO wa Kanda ya Afrika, pia alisisitiza umuhimu wa kuwa waangilifu zaidi juu ya janga jipya linalowezekana, licha ya kumalizika kwa janga hilo.

Wakati jumla ya kesi 12 zilirekodiwa wakati wa wimbi la 12 la janga, watu 6 walifariki.

Kesi ya kwanza ya kuzuka kwa janga ilionekana mnamo Februari 7 katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi.

Hivi sasa, Guinea inabaki kuwa nchi pekee ambayo janga la Ebola lilikuwa linaendelea.

Post a Comment

0 Comments