China yailaumu Marekani kwa kukwama kwa uhusiano wao

 


China imeilaumu Marekani kwa kile ilichokitaja "kukwama" kwa uhusiano wa nchi hizo mbili, katika mazungumzo ya ana kwa ana yaliyoanza hii leo kwenye mji wa China wa Tianjin. 

Makamu wa Waziri wa Mambo ya nje Xie Feng ameitaka Marekani ibadilishe kile alichokiita "fikra potofu na sera za hatari,” kulingana na ripoti za Shirika la Habari la Xinhua. 

Shirika hilo la Xinhua limemnukuu Xie akimwambia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Wendy Sherman kwamba uhusiano wa nchi zao umekwama kutokana na kwamba Marekani inaijengea sifa mbaya China na kuinadi kama adui wake. 

Aidha inaripotiwa kuwa huenda Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa China Xi Jinping wakakutana pembezoni mwa mkutano wa G-20 huko mjini Roma, Italia, mwishoni mwa Oktoba.


Post a Comment

0 Comments