https://monetag.com/?ref_id=TTIb DPP amfutia Mashtaka anayedaiwa kumteka Mo, Aachiwa huru na kukamatwa tena | Muungwana BLOG

DPP amfutia Mashtaka anayedaiwa kumteka Mo, Aachiwa huru na kukamatwa tena

 


MKURUGENZI wa mashtaka Nchinj, DPP amemuondolea mashtaka dereva taxi, Mousa  Twaleb anayedaiwa kumteka Mfanyabiashara Mohammed Dewji  'Mo', kwa sababu hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake.

Mapema upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Ester Martin ulidai mahakani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi dhidi ya Twelib leo Julai 26, 2021 iliitwa mahakakani hapo kwa ajili ya kutajwa lakini DPP aliwasilisha hati ya kuiondoa kesi hiyo (Nolle Prosequ) chini ya kifungu cha sheria cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai

Kufuatia hati hiyo Mahakama ikamuachia huru mshtakiwa. Hata hivyo, mshtakiwa Twelib baada ya kutoka tu nje ya chumba cha mahakama alikamatwa na askari.

Katika kesi hiyo inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, 2018, katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg Afrika Kusini, kwa makusudi mshtakiwa aliendesha genge la uhalifu.

Pia, inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo Hoteli ya Colloseum  wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Inadaiwa Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha kiasi cha Sh. Milioni nane wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

MO alitekwa nyara Oktoba 11, mwaka jana alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

Post a Comment

0 Comments