Nigeria yamchunguza afisa mkuu wa polisi kuhusu madai ya FBI katika kesi ya Hushpuppi

Polisi wa Nigeria wanasema wamepokea ‘madai ya na mashtaka’ Ofisi ya shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) dhidi ya afisa mwandamizi wa polisi.

Taarifa ya msemaji wa polisi Frank Mbah haikutoa maelezo ya madai dhidi ya Naibu Kamishna wa Polisi Abba Kyari, lakini ilisema waliamuru uchunguzi wa ndani wa afisa huyo kufuatia kupokelewa kwa michakato ya mashtaka.

Bw Kyari - ambaye ni polisi anayesifika nchini Nigeria kwa juhudi zake katika kuongoza mapambano dhidi ya uhalifu - ameripotiwa sana kuhusishwa na kesi ya ulaghai na utapeli wa pesa dhidi ya mshawishi wa mitandao ya kijamii wa Nigeria Ramon Abbas - anayejulikana pia kama Hushpuppi.

Nyaraka za korti zilizowasilishwa katika korti ya Marekani a zilisema uhalifu wa Hushpuppi uliwagharimu wahasiriwa wake karibu $ 24m (£ 17m) kwa jumla na amekiri mashtaka ya utapeli wa pesa.

Lakini Bw Kyari amekana kuhusika na udanganyifu au ufisadi kwa kushirikiana na Hushpuppi mwenye umri wa miaka 37, akielezea madai hayo kama '' uwongo '' na kusema mikono yake '' ni safi ''.

Siku ya Alhamisi, polisi wa Nigeria walisema wamejitolea kwa "'kufuata haki" na kuimarisha uhusiano wake na washirika wa kimataifa.

Post a Comment

0 Comments