JB atangaza kuacha kuigiza


Msanii wa  filamu za kibongo Jacob stephene maarufu kama JB ametangaza kuacha kuigiza na kufanya kazi hiyo ya sanaa akiwa nyuma ya kamera.

 JB ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa "Niliwahi kusema napumzika kufanya filamu na nitabaki kwenye tamthilia..lakini sasa Nafikiria kupumzika pia kuigiza na nitabakia nyuma ya camera kama Producer na Director
Tamthilia yangu ya #mwanamuzikiseries nafikiri itakuwa ndio ya mwisho..kuigiza..
Ni matumaini yangu kwenye kipindi chote
Tangu 1997 wakati naanza mambo hayo mpaka 2000 wakati naanzisha Jerusalem films umefurahia kazi zangu..lakini nakuahidi huo ni mwanzo tu..mengi mazuri yanakuja nikiwa nyuma ya camera.."

Post a Comment

0 Comments