Korea Kaskazini yajaribu kombora jipya la masafa marefu lenye uwezo wa kupiga Japan



Korea Kaskazini imefanya jaribio la kombora jipya la masafa marefu linaloweza kupiga sehemu kubwa ya Japan, vyombo vya habari vya serikali vimesema Jumatatu.

Jaribio lililofanywa mwishoni mwa wiki lilishuhudia makombora yakisafiri hadi umbali wa km1,500 (930 maili),kulingana na KCNA.

Jaribio hilo halikiuki maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa - lakini yalisababisha vikwazo vikali kwa Korea Kaskazini hapo zamani.

Lakini inaonesha kuwa nchi hiyo bado ina uwezo wa kutengeneza silaha licha ya upungufu wa chakula na changamoto za uchumi.

Jaribio la kombora la baharini linatoa "umuhimu wa kimkakati wa kumiliki kigingi kingine ni katika kuhakikisha usalama wa nchi yetu na nguvu za kijeshi dhidi ya vikosi vyenye uhasama," KCNA ilisema.

Jeshi la Marekani limesema kuwa jaribio hilo lilionesha "Korea Kaskazini inaendelea kuzingatia kukuza programu yake ya kijeshi na vitisho ambavyo vinapeleka kwa majirani zake na jamii ya kimataifa".

Iliongeza kuwa inazingatia kwa dhati nia yake ya kutetea washirika wake Korea Kusini na Japan.

Uchambuzi wa Laura Bicker wa BBC

Sababu ambayo wengine wanaweza kukataa jaribio hili la kombora ni kwa sababu ilikuwa kombora la kusafiri. Kombora la aina hii haliko chini ya vikwazo vya Baraza la Usalama la UN ambavyo viko katika kuzuia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Wengine wanaweza kuona hatua hii kama uchochezi wa chinichini kutoka Pyongyang - labda kujaribu ili kuona ni athari gani itakayotokea. Hakika haikuwa taarifa kubwa huko Korea Kusini, wala haikuwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la serikali la Korea Kaskazini.

Ugomvi wa nini?

Shida ni kwamba Korea Kaskazini inathibitisha tena kwamba inaweza kutengeneza silaha mpya na hatari licha ya kuwa na vikwazo vikali vya kimataifa.

Makombora haya ya kusafiri kwa ndege huruka chini na ni ngumu kugundua, na umbali wa km 1,500 ingeweka sehemu kubwa ya Japani katika hatari ya kulengwa.

Vyombo vya habari vya serikali pia vinaelezea makombora haya kama "mkakati" ambapo kwa kawaida inamaanisha kuwa serikali inatarajia kuweka silaha ya nyuklia juu yake.

Wachambuzi bado hawajui ikiwa Korea Kaskazini inaweza kutumia silaha ya nyuklia kwenye kombora la masafa. Hatahivyo, kutokana na kiasi cha maendeleo ambacho serikali ya siri imefanya hadi sasa, hakuna mtu atakayepinga.

Pyongyang inaweza kuwa kimya tangu mazungumzo kati ya Donald Trump na Kim Jong-un yalipovunjika huko Hanoi mnamo 2019.

Lakini haimaanishi watengenezaji wa silaha zao hawajishughulishi.

Vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vimepiga marufuku Korea Kaskazini kujaribu makombora, ambayo yanachukuliwa kuwa ya kutishia zaidi.

Korea Kaskazini ilijaribu makombora kama hayo mwezi Machi, hatua ambayo ilisababisha kukemewa vikali na Marekani, Japan na Korea Kusini.

Jaribio la sasa limekuja siku chache baada ya gwaride la kijeshi lililopunguzwa huko Pyongyang kufanyika kuadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwa serikali ya kikomunisti.

Haikuonesha makombora yoyote makubwa ya balistiki, lakini haswa ilionesha wafanyakazi katika suti za hazmat, ambayo inaweza kuwa ishara kwamba kikosi maalum kiliundwa kusaidia kuzuia kuenea kwa Covid-19.

Kuanzia tarehe 19 Agosti, Korea Kaskazini haikuwa imerekodi maambukizi ya Covid-19, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema - ingawa wakosoaji wanasema hii haiwezekani.

Nchi hiyo ilifunga mipaka yake mnamo Januari 2020 ili kuzuia kuenea kwa virusi, na kusababisha biashara na mshirika wake mkubwa wa uchumi China kuporomoka.

Tangu wakati huo kiongozi Kim Jong-un amekiri kwamba nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa chakula, huku kukiwa na ripoti kutoka kwa mashirika ya misaada kuwa watu wanakufa kwa njaa na uchumi unaozorota.

Lakini mipango yake ya nyuklia haijapunguzwa. Mwezi uliopita Shirila la kimataifa la nguvu atomiki la Umoja wa Mataifa lilisema kwamba nchi hiyo ilionekana kuanzisha tena mitambo ambayo inaweza kutoa plutonium kwa ajili yasilaha za nyuklia, na kuita maendeleo "yanayotia hofu sana".

 

Post a Comment

0 Comments