Msajili wa vyama vya siasa kukutana na kufanya kikao na wadau wa siasa pamoja na Jeshi la Polisi Septemba 23, 2021

Ili kujenga maelewano kwa wadau mbalimbali wa siasa na Jeshi la Polisi nchini OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeweka mpango mkakati wa kuandaa vikao vya wadau hao na Jeshi hilo kwa lengo la kuondoa changamoto zinazojitokeza baina yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amesema nia ya vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama Siasa.


Jaji Mtungi amesema kikao cha kwanza Cha wadau kitafanyika Septemba 23 mwaka huu ambapo ofisi hiyo itakutana na Jeshi la Polisi nchini kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

Vilevile amesema kuwa Octoba 13 mwaka huu baraza la vyama siasa litafanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar ambapo utashirikisha wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa.

“Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye anamafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano”amesema

Vikao hivi vinakuja ikiwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia.

 

Post a Comment

0 Comments