https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ndejembi atoa onyo kwa Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwa mazoea | Muungwana BLOG

Ndejembi atoa onyo kwa Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwa mazoea

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku pia akiwaasa kuepuka umungu mtu pamoja na kuwa waadilifu kazini.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Watumishi wa Manispaa ya Moshi na Halmashauri ya Moshi akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.


" Wapo watumishi wa umma wamekua wakifanya kazi kwa mazoea, unakuta mtu anafika kazini lakini hasikilizi changamoto za wananchi badala yake yupo bize na shughuli zake binafsi, Serikali haikatazi mtu kuwa na biashara zake binafsi lakini tunahitaji kwanza waweke maslahi ya wananchi ndio biashara zao zifuate," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Amesema kwa miezi kadhaa kumekua na watumishi wa umma ambao wanafanya kazi kwa mazoea na kushindwa kuishi falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Kazi Iendelee ambapo amesema Serikali haitomvumilia mtumishi yeyote ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake.

" Watumishi wengine wamejiweka miungu watu wanataka waogopewe, unaogopewa kwa kipi? Wakati wewe kazi yako ni kutumikia, Niwaeleze ukweli Serikali ya awamu ya sita haiwezi kuvumilia hawa wote wanaojifanya miungu watu, tunataka mshughulike na changamoto za wananchi wetu ambaye atashindwa tutamshughulikia yeye.

Hakuna kipindi kizuri cha kuwa mtumishi wa umma kama kipindi hiki cha Rais Samia, ameonesha kwa dhati nia yake ya kuboresha watumishi wa umma, Madaraja yalikua yamesimama lakini muda mfupi tokea aingie madarakani amepandisha madaraja na kutoa ajira mpya, tumlipe Rais wetu kwa kufanya kazi kwa kasi zaidi," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

 

Post a Comment

0 Comments