Ulaya yalaani vitisho kabla ya uchaguzi Urusi

 


Umoja wa Ulaya umekosoa kile ilichokiita hali ya vitisho kabla ya uchaguzi wa bunge nchini Urusi na umesema ukosefu wa waangalizi huru wa uchaguzi. 

Msemaji wa masuala ya kigeni wa umoja huo, Peter Stano amesema kile walichoshuhudia katika uchaguzi ni mazingira ya vitisho kwa wakosoaji wote huru. 

Uchaguzi huo wa siku tatu uliokamilika jana, umekipa chama tawala cha Rais Vladmir Putin ushindi mkubwa, licha ya utafiti wa maoni kuonesha kuporomoka kwa uungwaji mkono wa chama hicho. 

Vyama vya upinzani vimedai kuwepo udanganyifu mkubwa na Stano amewaambia waandishi habari kwamba Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuhusu ripoti zinazotolewa na waangalizi wa ndani. 

Amesema hapakuwa na waangalizi huru wa kimataifa, hivyo ni vigumu sana kuona jinsi uchaguzi ulivyofanyika. 

Waangalizi huru wa ndani wameripoti kuwepo kwa dosari nyingi wakati wa uchaguzi huo.


Post a Comment

0 Comments