https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ushirikiano wa KOSGEB na SMIDA kukuza kiwanda Zanzibar | Muungwana BLOG

Ushirikiano wa KOSGEB na SMIDA kukuza kiwanda Zanzibar


Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali itakamikisha na kutekeleza Mkataba wa Makubaliano kati ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo na Biashara ndogo na za kati (KOSGEB) la Uturuki na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) la Tanzania  kwa lengo la kuipatia SIDO mafunzo na uzoefu katika kuboresha utoaji msaada na uwezeshaji wa Viwanda na Biashara ndogo na za kati (SMEs).
 
Prof. Mkumbo amesema hayo alipotembelea KOSGEB akiwa ameambatana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar Omar Shaaban pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Mazingira David Makiposa, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Hassani Mwamweta na Maafisa wa Wizara ili kujifunza na kupata uzoefu wa jinsi ya kuboresha huduma zinazotolewa na SIDO ya Tanzania kwa SMEs.


Prof. Mkumbo na ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea baadhi ya viwanda vidogo vinavyowezeshwa na KOSGEB na walifurahishwa na usimamizi na maendeleo ya viwanda hivyo katika utengenezaji ya bidhaa kwa kutumia ubunifu na teknolojia zinazokidhi mahitaji ya soko kimataifa.
 
Naye  Mkurugenzi Mkuu wa KOSGEB Hassan Basri Kurt alimueleza Waziri Mkumbo na ujumbe wake kuwa Shirika hilo liko tayari kukamilisha Mkataba wa Makubaliano na SIDO ya Tanzania na kuanzisha Mkataba na Wakala wa Viwanda Vidogo vidogo, na vya Kati (SMIDA) ya Zanzibar.

KOSGEB ina mikataba ya makubaliano 93 katika taasisi 88 katika nchi mbalimbali 69 pamoja na mashirika ya kimataifa matano hivyo iko tayari kukamikisha makubaliano na SIDO ya Tanzania ambayo yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments