https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wananchi wahimizwa kujifunza kuogelea | Muungwana BLOG

Wananchi wahimizwa kujifunza kuogelea

Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Saimon sirro ametoa rai kwa wananchi wanaoishi Kando Kando ya mto ,ziwa na bahari kupata mafunzo ya usalama majini katika chuo cha polisi wanamaji Mkoani Mwanza ilikusaidia kupunguza ajali za majini.

IGP Sirro ametoa rai hiyo wakati akizungumza na maofisa wa polisi jijini Mwanza katika kikao kazi chenye lengo la kuimalisha utendaji kazi.

Aidha IGP Sirro amesema kuwa wavuvi na wadau wengine wanaotumia vyombo vya majini watajengewa uwezo wa kukabiliana na ajali za majini ili kuweza kufanya shughuli zao kwa amani.


"Wanaotaka kujifunza mambo ya baharini basi waje kwenye chuo chetu cha hapa Mwanza kimekubalika katika Nchi kumi na nne ndio kiwe chuo chetu cha kutoa mafunzo kwenye swala la wananmaji nichuo kizuri kinavifaa vya kutosha kwahiyo niwaombe waje wajifunze na nimeisha toa maelekezo ya kutosha mafunzo yatakuwa ya bei nafuu sana nI jambo la aibu kama safari yako unapita majini alafu hujui kuogelea namna ya kuvaa majaketi ya kuogelea amesema Igp Sirro.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha polisi wanamaji Mwanza Kamishina Msaidizi wa polisi Ndagile makubi amesema kuwa mafunzo wanayoyatoa yatasaidia kuleta manufaa kwa wavuvi na wanaojihusisha na kaziza ziwani.

Makubi amesema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya wanamaji kwa askari wa jeshi la polisi na kwa watumishi wa taasisi za umma na binafsi na kwa mtu mmoja mmoja, mafunzo yanatokea ni ya usala majini ambayo yanahisisha kuoa watu majini

Majanga makubwa yamekuwa yakitokea ziwani na baharini na watu wengi wanapotea maisha   hii ni kwasababu watu wengi hawana ujuzi wakujiokoa pindi majanga hayo yanapotokea, hivyo  chuo kimetoa fursa kwa mtu yoyote kuja kupata mafunzo ya kuogelea na mafunzo ya uzamiaji.

Alisema kuwa chuo hicho kinavifaa vya kutosha na uzoefu mkubwa wa kufundishia watu mbinu mbalimbali za kujiokoa pindi wanapokuwa ziwani.

 

Post a Comment

0 Comments