Nov 24, 2021

ECDC yatoa wito wa kuimarishwa kwa haraka hatua za kukabiliana na corona

  Muungwana Blog       Nov 24, 2021


Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya ECDC kimetoa wito kwa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya kuanzisha hatua za kupunguza uwezekano wa matatizo makubwa yanayotokana na ugonjwa wa Covid-19 katika mwezi wa Desemba na Januari. 


Mkuu wa kituo hicho cha ECDC Andrea Ammon, amependekeza chanjo ya ziada kwa watu wazima walio na umri wa zaidi ya miaka 18 huku kipaumbele kikitolewa kwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 40.


 Shirika hilo pia limeyahimiza mataifa kuongeza viwango vyao vya chanjo kwa ujumla, haswa yale yalio na viwango vya chini. ECDC imesema chini ya asilimia 70 ya idadi kamili ya watu katika Umoja wa Ulaya na eneo la kiuchumi la Ulaya wamepata chanjo hali inayoacha pengo kubwa la chanjo ambalo haliwezi kuzibika kwa haraka na hivyo basi kutoa nafasi ya kuenea kwa virusi.

logoblog

Thanks for reading ECDC yatoa wito wa kuimarishwa kwa haraka hatua za kukabiliana na corona

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment