Papa atoa wito wa kuwasaidia wahamiaji


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amezitolea wito serikali duniani kote kuongoza jitihada katika kuwasaidia wahamiaji na wakimbizi, huku akitangaza kusitisha ibada kutokana na kasi ya ongezeko la maambukizo ya virusi vya corona.


Kauli hiyo ya Papa Francis katika kanisa kuu la Mtakatifu Petro ilionekana kuzilenga serikali na majeshi, huku akielezea kuhuzunishwa na vifo vilivyotokea katika eneo la mlango bahari wa kuingia Uingereza, mpaka wa Poland na Belarus pamoja na Bahari ya Mediterania.


Papa Francis ana mpango wa kwenda Cyprus na baadaye Ugiriki, katika ziara ambayo imepangwa kuanza Alhamis, ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kukutana na wakimbizi.

Post a Comment

0 Comments