ILO - zaidi ya Waafghani nusu milioni wamepoteza ajira sababu ya Taliban

 


Shirika la Kazi Duniani ILO limesema zaidi ya nusu milioni ya Waafghani wamepoteza kazi zao baada ya Taliban kuchukua madaraka mwaka uliopita. 

Katika ripoti mpya iliyotolewa leo, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema idadi ya ajira zilizopotea huenda zikafikia laki tisa ifikiapo katikati ya mwaka 2022. 

Ramin Behzad ambaye ni mshirikishi mwandamizi wa ILO amesema hali ni mbaya mno Afghanistan na msaada wa haraka kwa ajili ya kufufua ajira unahitajika. 

Mamia ya Waafghani hasa wanajeshi, majaji na wanawake waliachishwa kazi baada ya Taliban kuchukua mamlaka baada ya majeshi ya kimataifa kuondoka nchini humo mnamo Agosti mwaka uliopita.


Post a Comment

0 Comments