https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mahakama ya Ubelgiji yamhukumu miaka 15 jela mlanguzi wa watu | Muungwana BLOG

Mahakama ya Ubelgiji yamhukumu miaka 15 jela mlanguzi wa watu

 


Mahakama moja nchini Ubelgiji leo imemhukumu mtu mmoja raia wa Vietnam miaka 15 jela baada ya kumpata na hatia ya kuwa kiongozi katika ulanguzi wa wahamiaji 39 waliopatikana wamefariki dunia kwenye lori. 

Vo Van Hong mwenye aliye na umri wa miaka 45, amepatikana na hatia ya kuongoza operesheni ya ulanguzi wa watu inayohusishwa na lori moja lililopatikana limesheheni miili ya watu katika mtaa mmoja nchini England Oktoba mwaka 2019. 

Kugunduliwa kwa miili hiyo katika mtaa huo wa London Mashariki ni moja ya visa vibaya zaidi vinavyowahusu wahamiaji katika miaka ya hivi karibuni. 

Wahanga hao, wanaume 31 na wanawake 8 kati ya umri wa miaka 15 hadi 44 wote walikuwa raia wa Vietnam na walifariki kutokana na kukosa hewa ya kupumua na joto kupita kiasi, kutokana na nafasi ndogo iliyokuwa katika lori hilo lililowasili England kwa njia ya feri.


Post a Comment

0 Comments