Mwandishi wa Uganda akamatwa tena muda mfupi baada ya kupata dhamana

Mwandishi wa Uganda aliyekuwa akizuiliwa Kakwenza Rukirabashaija amekamatwa tena, muda mfupi baada ya kuachiwa kutoka gerezani, licha mahakama katika mji mkuu Kampala kumpatia dhamana.

Mwandishi huyo amefikishwa maha kupiatia video-link, kutoka gerezani.

Kama sehemu ya masharti ya dhamani, mahakama ilimuamuru asisafiri nje ya nchi na kuwasilisha pasipoti yake mahakamani kwa miezi sita.

Pia amezuiliwa kuzungumzia hadharani kesi dhidi yake.

Lakini Wakili wake Eron Kiiza, anasema wanaume ambao hawakuwa wamevalia sare za polisi walimkamata mara alipokanyaga nje ya gereza Jumanne mchana, kumrusha kwenye gari aina ya pickup ambalo halikuwa na nambari ya usajili na kuondoka naye.

Mwandishi huyo ambaye amekuwa kizuizini kutoka mwezi Disemba mwaka jana mara ya kwanza alizuiliwa kisiri na vikosi vya usalama, na baadaye kuwekwa rumande gerezani mapema mwezi huu.

Mawakili wake waliomba dhamana kwa sababu za kimatibabu wiki iliyopita, kutokana na ripoti ya Jeshi la Magereza iliyosema kuwa Bw. Rukirabashaija alikuwa na makovu yanayoponya katika baadhi ya sehemu za mwili wake.

Ripoti ya daktari wa Magereza iliongeza kuwa alipata majeraha kabla ya kuhamishwa chini ya ulinzi wao.

Mawakili wa Bw. Rukirabashaija wamesema kuwa mwandishi huyo aliteswa akiwa kizuizini.

Anakabiliwa na mashtaka mawili ya mawasiliano ya kukera, chini ya Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta, kuvuruga amani ya Rais Museveni na mwanawe Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kamanda katika jeshi. Alikana mashitaka hayo.

Bw. Rukirabashaija alishinda tuzo ya ya Kimataifa ya PEN Printer ya mwandishi mwenye wa ujasiri mwaka wa 2021, kupitia riwaya yake "The Greedy Barbarian" ambayo inachunguza mada ya ufisadi mkubwa.

 

Post a Comment

0 Comments