Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Baada ya Vitisho vya Urusi, Hatimaye Finland Yatangaza Kujiunga NATO

 

RAIS wa Finland Sauli Niinisto ametangaza nchi yake kujiunga na Jumuiya ya Umoja wa kujihami wa Mataifa ya Magharibi (NATO), Finland inapakana na Urusi na kwa mujibu wa taratibu nchi hiyo inabidi iandike maombi rasmi ya kujiunga na Umoja huo.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sanna Marin imesema:

“Tunadhani kuwa hatua za kitaifa inabidi zichukuliwe mapema na kwa uharaka ndani ya siku chache zijazo.”

Tangu Urusi ichukue eneo la Crimea mwaka 2014 Finland imezidisha uhusiano na Jumuiya ya NATO kama mshirika mwenza, lakini ilikuwa bado haijajiunga kama sehemu ya kulinda uhusiano wake na mataifa ya Ulaya Mashariki.

Ndani ya muda mchache ujao Serikali na Bunge la Finland linatarajiwa kuidhinisha mchakato huo.

Mnamo mwezi uliopita Rais Niinisto akiongea na Gazeti la IIta-Sanomat:

“Kama itatokea na inavyoonekana itatokea, kwa Finland na Sweden kujiunga na NATO, itatutengenezea uhusiano imara na wenye nguvu.”

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Shirika la Utangazaji la Umma YLE zimeonesha kuwa 76% ya raia wa Finland wanataka nchi yao ijiunge na NATO huku 12% wao wakigoma nchi yao kujiunga na NATO, 12% wao hawafungamani na upande wowote.

Rais wa Finland Sauli Niinisito akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin

Kwa upande mwingine Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson hivi karibuni alitembelea miji mikuu ya Finland na Sweden ya Stockhol na Helsinki na kusaini makubaliano ambayo yanadai Uingereza itaingilia kati na kutoa msaada endapo nchi hizo zitavamiwa na adui, vivyo hivyo kwa upande wa Sweden na Finland nazo zitaingilia kati na kutoa msaada endapo Uingereza itavamiwa na adui.

Kwa muda mrefu Urusi imekuwa ikizipiga marufuku nchi za Sweden na Finland kujiunga na NATO, lakini kwa hatua hii inayochukua Finland ni wazi imekaidi onyo la Urusi hivyo kinachosubiriwa ni kuona namna gani Urusi itafanya juu ya uamzui huu wa Finland.

Post a Comment

0 Comments