Ticker

6/recent/ticker-posts

 


G7 yaahidi kuisaidia Ukraine hadi ipate ushindi


Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani, G7, wameahidi kuisaidia Ukraine katika vita vyake na Urusi, huku Umoja wa Ulaya ukiahidi kuongeza msaada kwa Ukraine kwa zaidi ya dola nusu bilioni. 


Mawaziri hao wamekutana leo katika mkutano wao wa siku tatu nchini Ujerumani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian amesema kundi la G7 limeungana zaidi katika nia yao ya kuendelea kwa muda mrefu kuisaidia Ukraine kupigania uhuru wake hadi itakaposhinda. 


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema umoja huo umeahidi kutoa euro milioni 500 zaidi kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Fedha hizo zitaongeza jumla ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya kwa Ukraine na kufikia euro bilioni mbili.

Post a Comment

0 Comments