NATO: Uturuki yahimiza hatua madhubuti kutoka Sweden, Finland


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Sweden na Finland lazima sasa zichukue hatua madhubuti ili kupunguza wasiwasi wa usalama wa nchi yake na kuondoa pingamizi la Ankara kwa ombi lao la uwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO. 


Wajumbe kutoka nchi hizo mbili za kaskazini mwa Ulaya wamerejea nyumbani wakiwa na nyaraka zinazoelezea wasiwasi wa Uturuki, kama vile taarifa kuhusu makundi ya ugaidi, baada ya ziara ya wiki hii na Ankara inasubiri majibu yao. 


Cavusoglu amesema Uturuki inaelewa wasiwasi wa usalama wa Finland na Sweden lakini kila mmoja pia anahitaji kuelewa kuhusu wasiwasi halali wa usalama wa Uturuki. Sweden na Finland ziliwasilisha maombi yao ya kujiunga na NATO wiki iliyopita. 


Hatua hiyo inadhihirisha mojawapo ya athari kubwa kabisa za siasa za kikanda za vita vya Urusi nchini Ukraine na huenda ikaichora upya ramani ya usalama barani Ulaya.

Post a Comment

0 Comments