Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Wazazi nchini India wanamshtaki mtoto wao kwa kutowapatia mjukuu

 


Wazazi wawili nchini India wanamshtaki mtoto wao wa kiume kwa kutowapatia mjukuu.


Wanandoa katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttarakhand wameshtaki mtoto wao wa pekee wa kiume na mke wake kwa kutowapatia mjukuu baada ya miaka sita ya ndoa.


Sanjeev 61 na Sadhana Prasad 57, wanasema walitumia akiba yao kumlea mtoto wao wa kiume, kulipia mafunzo ya urubani wake pamoja na harusi ya kifahari.


Wanadai fidia ya takriban $650,000 (£525,000) kama hakuna mjukuu anayezaliwa ndani ya mwaka mmoja.


Mtoto wao na mkewe hawajasema chochote kuhusiana suala hilo.


Kesi hiyo isiyo ya kawaida sana iliwasilishwa kwa misingi ya "unyanyasaji wa kiakili".


Bw Prasad alisema ametumia akiba yake yote kwa mtoto wake, na kumpeleka Marekani mwaka wa 2006 kwa mafunzo ya urubani kwa gharama ya $65,000.


Alirejea India mwaka wa 2007, lakini alipoteza kazi yake na familia yake ikalazimika kumsaidia kifedha kwa zaidi ya miaka miwili, gazeti la Times of India linaripoti.


Shrey Sagar, 35, hatimaye alipata kazi kama rubani. Wazazi wake wanasema waliandaa doa yake na Shubhangi Sinha, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, mwaka wa 2016, kwa matumaini kwamba watapata "mjukuu wa kucheza naye" wakati wa kustaafu kwao.


Wazazi hao wanasema walilipia sherehe ya harusi katika hoteli ya nyota tano, gari la kifahari la thamani ya dola 80,000 na fungate nje ya nchi.


“Mwanangu amekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita lakini bado hawajapanga kupata mtoto,” Bw Prasad alisema.


"Angalau ikiwa tuna mjukuu wa kukaa naye, maumivu yetu yatavumilika." Wakili wa wanandoa hao, AK Srivastava, aliambia The National kwamba wenzi hao walikuwa wamedai pesa hizo "kwa sababu ya ukatili wa kiakili".


"Ni ndoto ya kila mzazi kuwa babu na nyanya. Walikuwa wamesubiri kwa miaka mingi kuwa babu na nyanya." Ombi la wanandoa hao, lililowasilishwa Haridwar, linatarajiwa kusikilizwa na mahakama tarehe 17 Mei.

Post a Comment

0 Comments