bunge wa jimbo la Ndanda, aratibu mafunzo ya viuatilifu kwa wakulima wa korosho

 


Na Hamisi Nasri, Masasi. 

KAMPUNI ya Bens Agrostar ambao ni ndio wazamabazaji wa viuatilifu vya mazao mbalimbali ikiwemo zao la korosho kwa mikoa ya kusini wamewataka wakulima mikao hiyo kuzingatia matumizi sahihi ya viuatilifu hivyo pindi wanapoandaa mashamba yao ya mikorosho ikiwemo uchanganaji bora kabla ya kutumia lengo kuweza kuongeza tija katika zao la korosho kusini.


Wito huo umetolewa jana mjini Masasi na afisa kilimo wa kampuni hiyo, Frank Miti alipokuwa akitoa mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa viongozi mbalimbali wa kata kutoka jimbo la Ndanda, mafunzo hayo yameratibiwa na Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe kwa na kufadhiliwa na kampuni hiyo ya Agrostar kutoka jijini Dar es saalam

Miti amesema kuwa katika kutambua umuhimu wa matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima kampuni ya Bens ilifanya tafiti katika eneo hilo na kutambua kwamba wakulima wengi hawana elimu ya kutosha ya matumizi bora ya viuatlifu hivyo kushindwa kuwa na tija katika uzalishaji wa zao la korosho nchini.

Amesema kutokana na tafiti hiyo hivi sasa wao wamekuja kwa kutoa elimu pamoja na kuwasambazia viuatilifu bora wakulima ili zao la korosho katika mikoa ya kusini liendelee kuwa na tija zaidi na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Amesema kwamba katika eneo la kutoa mafunzo pia walijikita zaidi kwenye matumizi ya mashine za kupulizia ambazo pia zimeonekana kuwa ni changamoto kubwa kwa wakulima kufahamu jinsi ya kuzitumia kuanzia kuwasha pamoja na kuchanganya dawa hizo ambazo ni viuatilifu.

 Amesema kuwa mafunzo ambayo yanatolewa na Bens kwa wakulima yanamatarajia makubwa kwa wakulima kuweza kuongeza uzalishaji wa mazao ikiwemo zao la korosho ambalo ndilo kitovu kikubwa cha uchumi wa kusini na taifa kwa ujumla.

 Miti amesema kwamba kampuni ya Bens itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima ili kuhakikisha kila mkulima anapata elimu ya kutosha juu ya viuatilifu na mabomba na kuondokana na matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu hivy.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe amesema kuwa ameamua kuratibu mafunzo hayo baada ya kuona wakulima wengi nchini wanakabiliwa na ukosefu wa elimu ya matumzi sahihi ya viuatilifu hivyo kupitia elimu hiyo itaweze kuwasiaidia na kuongeza tija katika zao la korosho.

Post a Comment

0 Comments