https://monetag.com/?ref_id=TTIb Chama cha Conservative cha Uingereza chapoteza viti viwili vya bunge | Muungwana BLOG

Chama cha Conservative cha Uingereza chapoteza viti viwili vya bunge


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepata pigo mara mbili baada ya wapiga kura, kukiadhibu chama chake cha Conservative katika chaguzi mbili muhimu za bunge zilizogubikwa na hoja za utawala wake na maadili. 

Johnson alipata pigo jingine siku ya Ijumaa, baada ya mwenyekiti wa Conservative Oliver Dowden kutangaza kujiuzulu akisema nchi inahitaji uongozi mpya. 

Chama cha Liberal Democrats kilishinda viti viwili vya kijijini kusini mashariki mwa England vya Tiverton na Honiton, wakati chama kikuu cha upinzani cha Labour kikinyakua kiti cha Wakefield kaskazini mwa Uingereza kutoka chama cha Conservative chake Johnson. 

Uchaguzi huo ulifanyika baada ya wabunge Conservative waliokumbwa na kashfa za ngono kujiuzulu. Johnson alinusurika kuondolewa madarakani katika kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye.


Post a Comment

0 Comments