"Ifikie wakati kumiliki Ndege isiwe anasa"- Mdee

 


Mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee, amesema kwamba ifikie hatua Watanzania waache kufikiria kimaskini jambo ambalo litawafanya waone kwamba mtu kumiliki Ndege isiwe anasa.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 27, 2022, Bungeni jijini Dodoma.

"Lazima ifike kipindi kumiliki Ndege isiwe anasa, shida ni kwamba sometimes sisi Watanzania tunafikiria kimaskini sana, yaani Ester Bulaya au Mwigulu Nchemba kuwa na kale ka-charter cha abiria 14 ni kitu cha kawaida ili tushindanishe watu waruke huko hewani , watalii waje wabebwe lazima hii iwe mentality yetu, tusifikirie kimaskini," amesema Mdee

Post a Comment

0 Comments