Serikali yapunguza tozo ya ving’amuzi

 


Serikali imepunguza tozo ya ving’amuzi nchini kufikia Sh500 hadi Sh2000 kwa kadri ya matumizi ya mteja baada ya majadiliano na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Kabla ya majadiliano hayo tozo iliyopendekezwa katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya serikali 2022/23 ilikuwa Sh1,000 hadi Sh3,000.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 2022/2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Fedha 2022.

Amesema Serikali ilipendekeza Sheria ya Posta na Mawasiliano ya kuanzisha tozo hiyo ya Sh1,000 hadi Sh3,000 kwa ving’amuzi itakayokuwa ikitozwa kupitia malipo ya vifurushi.

“Hata, hivyo baada ya majadiliano ya kina ilionekana kwamba kiwango hicho ni kikubwa”amesema Sillo.

Amesema kamati ilipendekeza kuanza kutoza kati ya Sh500 hadi Sh2,000 na kwamba Serikali ilikubali pendekezo la Kamati.

Post a Comment

0 Comments