Ticker

6/recent/ticker-posts

Wakulima nchini wahamasishwa kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku


Wakulima Kijiji cha Ntokela kata ya Ndanto Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameanza kusajiliwa kwenye mfumo wa kidigitali wa mbolea ili waweze kunufaika na ruzuku ya mbokea itakayotolewa na serikali msimu wa kilimo wa mwaka 2022/2023


Usajili huo umeanza  jana tarehe 4 Julai, 2022 na timu iliyoambatana na  Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Michael Sanga na  kijijini hapo na kujionea  jinsi wananchi wanavyojitokeza  ili kusajiliwa.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kijijini hapo Sanga alisema, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 150 ili kuwapunguzia gharama ya mbolea wakulima nchini na kuwawezesha kulima kwa tija. 

Kwa upande wake Afisa Kilimo na mmoja kati ya wajumbe wanaosimamia utoaji wa mbolea ya ruzuku, Kisah Chawe alisema ili kunufaika na mbolea ya ruzuku sharti kusajiliwa.

Aliongeza taarifa muhimu wakati wa kusajiliwa ni pamoja na majina ya mkulima, kitambulisho, ukubwa wa shamba, aina ya mazao anayolima, na baadaye atapigwa pichwa na kuchukuliwa alama zake vidole.

Post a Comment

0 Comments