Wasiwasi waongezeka juu ya usalama wa kinu cha Zaporizhzhia


Wasiwasi unazidi kuongezeka juu ya usalama wa kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine katika wakati Urusi inaendeleza mashambulizi kusini na mashariki mwa Ukraine. 


Tangu jana hofu imetanda kuhusu uwezekano wa kuvuja kwa mionzi kutoka kinu hicho cha kufua umeme kwenye mkoa wa Zaporizhzhia unaodhibitiwa hivi sasa na vikosi vya Urusi. 


Wasiwasi huo unafuatia ripoti kwamba sehemu ya kinu hicho “imeharibiwa vibaya” kwa mashambulizi ya kijeshi na mtambo mmoja wa nyuklia umelazimika kuzimwa. 


Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky ameituhumu Urusi kuhusika na hujuma dhidi ya kinu hicho cha nyuklia ambacho ndiyo kikubwa kuliko vyote barani Ulaya. 


Mkuu wa shirika la Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA, Rafael Grossi, ametaka wataalamu wa shirika hilo wapatiwe nafasi ya kukifikia kinu hicho kuepusha kile amekitaja kuwa kitisho cha kutokea janga la nyuklia

Post a Comment

0 Comments