Zelensky asifu mafanikio ya jeshi la nchi yake dhidi ya Urusi


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kufanikiwa kuzidisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi nchini humo. Katika hotuba yake kwa njia ya video jana usiku, Zelensky amesema katika muda wa wiki moja iliyopita, jeshi la Ukraine lilipata mafanikio makubwa katika kuharibu mikakati ya jeshi la Urusi. 


Zelensky ameongeza kuwa kila shambulizi dhidi ya hifadhi ya risasi za Urusi, vituo vya kamandi yake na mkusanyiko wa vifaa vya Urusi linaokoa maisha ya wote na maisha ya wanajeshi na raia wa Ukraine.


Zelensky alikuwa akizungumzia mafanikio madogo ambayo jeshi la nchi hiyo limeyapata kwenye majimbo ya Kherson na Zaporizhzhia yaliyokamatwa na Urusi miezi ya hivi karibuni. Vikosi vya Ukraine vimemudu kuyakomboa baadhi ya maeneo ya majimbo hayo lakini sehemu kubwa ardhi ya mikoa hiyo bado inadhibitiwa na Urusi.

Post a Comment

0 Comments