https://monetag.com/?ref_id=TTIb Maelfu ya Wapalestina wafanya ibada kwa ajili ya waliopata ajali baharini | Muungwana BLOG

Maelfu ya Wapalestina wafanya ibada kwa ajili ya waliopata ajali baharini

 


Maelfu ya Wapalestina wamefanya ibada  katika uwanja mdogo wa kandanda katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Lebanon kwa ajili ya ajali mbaya ya baharini kuwahi kutokea katika muda mrefu ambapo wahamiaji wengi walipoteza maisha wiki hii wakati boti yao ilipozama katika pwani ya Syria


Mazishi ya Jumamosi yalifanyika huku idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo ya boti ya wahamiaji ikiongezeka na kufikia 89 na kuifanya kuwa mbaya zaidi kufikia sasa huku idadi kubwa ya watu wakikimbia Lebanon inayokumbwa na mzozo wa kiuchumi.


Jeshi la Lebanon lilitangaza kuwa wanajeshi wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kuandaa safari hiyo iliyouwa watu. Mzozo wa kiuchumi wa miaka mitatu wa Lebanon unachukuliwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani tangu miaka ya 1850 na kusababisha robo tatu ya nchi hiyo kuwa maskini.

Post a Comment

0 Comments