Ticker

6/recent/ticker-posts

Wanajeshi wa Cameroon wakamatwa kutokana na mauaji


Mamlaka za Cameroon zimesema Alhamisi kwamba zimezuilia wanajeshi watatu kutokana na kupiga risasi na kuuwa wanawake wawili wasiokuwa na silaha kwenye kijiji kimoja kaskazini magharibi mwa nchi.


Makundi ya kutetea haki za binadamu yanalaumu jeshi la Cameroon kwa kuuwa wanavijiji kwenye msako ambao umekuwa ukiendelea mwezi Septemba, wa kusaka washukiwa wanaopinga utawala , madai ambayo yamepingwa vikali na serikali. Jeshi la Cameroon limekiri kwamba wanajeshi wake wa tatu kutoka kikosi cha wanahewa wiki hii wameua wanawake wawili kwenye kijiji kinachotumia lugha ya kiingereza cha Nylbat kilichoko wilaya wa Andeck.


Taarifa iliyotiwa saidi na msemaji wa jeshi Serge Cyrill Atongfack inasema kwamba wanajeshi hao walikuwa wametumwa ili kupambana na wanamgambo kwenye eneo la kaskazini magharibi mwa nchi lililotatizika. Ripoti zinaongeza kusema kwamba walikaidi amri na kuanza kumiminia raia wa kawaida risasi, na ndipo wanawake hao wawili walipouwawa.

Post a Comment

0 Comments